Tangaza na Abd Da Hustler

Meli yenye Bhangi ilisajiliwa Zanzibar


Mmea wa Bhangi
Polisi nchini Tanzania wamethibitisha kuwa meli iliyokamatwa Jumamosi katika bahari ya Mediterranea ikiwa na mizigo ya Bhangi yenye thamani ya dola milioni sabini na nane, ilikuwa imesajiliwa Zanzibar.
Wafanyakazi tisa waliokuwa kwenye meli hiyo wanaosemekana kuwa raia wa Misri na Syria, waliwasha moto meli hiyo na kuruka baharini, ingawa baadaye waliokolewa.
Maafisa wa ushuru wa Italia walioinasa meli hiyo iliyokuwa kwenye ufuo wa Sicily baada ya kupata taarifa, walisema kuwa
mizigo iliyokuwa na mizigo ya Bhangi yenye tani thelathini, ilipakiwa kwenye meli hiyo bandarini Uturuki ingawa haijulikani ilikokuwa inapelekwa.


Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment