Kuna takribani magonjwa 25 ya zinaa ambayo kila mojawapo huwa na dalili
zake tofauti na lingine, watu huambukizana bila kujua, isipokuwa kwa mtu
mwenyewe kujitambua kuwa amekwisha ambukizwa.
Mara nyingi ugonjwa huu huambukizwa kwa kwa kufanya mapenzi bila kinga,
kunyonyana ndimi (denda) na kushika shika nyeti. Ugonjwa huu huenea
kimia kimia kwa wingi siku hizi, kutokana na watu kutokuwa na elimu
kuhusu ugonjwa huu. Hapa unaweza kuona ukweli na uwazi kuhusu ugonjwa huu, nahivyo utaweza kujikinga au kuwahi hospitali kupata tiba mbadala.
Kwanza, Ugonjwa wa zinaa ambao kitaalamu hufahamiaka kama sexul
transmitted disease (STD) ni ugojwa ambao huambukizana watu wanapokuwa
wanafanya tendo la ngono linalokutanisha nyeti zao au kufanya mapenzi
kwa aina yoyote ile kama kunyonyana ndimi.Pia magonjwa kama HIV/AIDS
huambukizwa kwa kuchangia sindano na vitu vingine vyenye ncha kali.
Pili, Kama mtu amekwisha ambukizwa ugonjwa wa zinaa na bado
hajaona madhara au dalili yoyote ya ugonjwa huo, bado akifanya mapenzi
na mpenzi wake bila kutumia kinga, anaweza kumuambukiza ugonjwa huo
mpenzi wake. Hata hivyo kwa ujumla watu hawawezi kutambua kama
wameambukizwa ugonjwa huu kama hawajaona dalili zozote za ugonjwa
huo.Unashauriwa endapo utakuwa na mashaka kuwa umeambukizwa, nenda
haraka katika kituo cha afya kilichopo jirani yako ukapimwe na uanze
kutumia dawa utapona kabla ya kupata madhara makubwa.
Tatu, Njia pekee ya kuepuka kupata maambukizi na madhra ya
ugonjwa huu wa zinaa, ni kutofanya mapenzi na mwanamke au mwanaume
mwenye ugonjwa huu au kutumia kondom.Kuna aina mbali mbali za kondom
ambazopatikana katika madukani, kwa mfano kuna kondom za kike na za
kiume. Kumbuka kuwa vidonge vya mpango wa uzazi vinaweza kuzuia kupata
mimba tu, havizuii kupata maambukizo ya magonjwa ya zinaa. Ushauri wa
mwisho, kama umekwisha ambukizwa ugonjwa huu na umepata maelekezo ya
kutumia dawa na daktari, basi hakikisha unamaliza dozi yote na kuwa
karibu na dokta kwa matibabu ya ziada.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 MAONI :
Post a Comment