Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia (Amison),
kwa ushirikiano na wahisani wake, umeanza mkutano hii leo na washirika
wake mjini Mombasa Pwani ya Kenya kuhusu kuchangia habari na taarifa
muhimu.
Lengo la mkutano huo ni kubuni mpango
utakaowezesha nchi zilizochangia wanajeshi kwa AMISOM kuchangia taarifa
mara kwa mara kati ya Amisom, mashirika ya usalama nchini Somalia na
mashirika mengine ya kikanda .
Akiongea wakati wa sherehe ya ufunguzi wa
mkutano huo, mjumbe maalum wa muungano wa Afrika nchini Somalia,Mahamat
Saleh Annadif aliwakumbusha washirika kuwa vitendo vya kigaidi
vinavyofanywa nchini humo havina mpaka.Kwa hivyo, vita dhidi ya ugaidi lazima vifanywe kwa mpangilio unaofaa. Baada ya kukabiliwa na changamoto nyingi, kundi la Al-Shabab limeanza kubuni njia mbadala za kupambana na maadui wake kwa kukusanya taarifa za kijasusi.
Mkutano huu unatarajiwa kuangazia kwa kina hali inayokumba Somalia hususan vitendo vya kigaidi, uhalifu wa kupangwa na kuongezeka kwa idadi ya silaha ndogondogo
Pia unalenga kuimarisha miundo mbinu ili kuwezesha nchi kuchangia taarifa wakati wote pamoja na mengi mengineyo.

0 MAONI :
Post a Comment