Tangaza na Abd Da Hustler

BREAKING NEWS: CHELSEA WATOA OFA PAUNDI MIL. 10 NA MCHEZAJI MMOJA KATI MATA AU LUIZ ILI KUMSAJILI WAYNE ROONEY


Manchester United imeikataa ofa ya Chelsea kumsajili mshambuliaji Wayne Rooney na kuwaambai Chelsea wasirudi na ofa nyingine yoyote ya kumtaka Rooney.
Chelsea ilitoa ofa ya paundi milioni 10 pamoja na mchezaji mmoja kati ya Juan Mata au David Luiz, kwa mujibu wa BBC, Man United iliikataa mara moja ofa hiyo mara tu baada ya kuipata na kusisitiza Rooney hauzwi. 
Rooney jana aliripotiwa kuwa na hasira kwa namna anavyotendewa na klabu yake, baada ya kauli za mabosi David Moyes na Ed Woodward.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amekuwa muwazi wa hisia zake juu ya kumhitaji Rooney kwenye kikosi chake, lakini David Moyes amesisitiza kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Everton hauzwi. 
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment