Wewe Mwanaume Unayesoma Hapa, Jiulize; Huwa Unadumu Na Mwenzi Wako?
Unaachwa Au Kukimbiwa Baada Ya Muda Mfupi? Kama Jibu Ni Ndiyo, Hapa
Utapata Tiba. Sikia Nikuambie, Wapo Wengi Ambao Kila Wakianzisha
Uhusiano, Siku Mbili Tatu, Mwanamke Anamkimbia.
Anampenda Sana, Anamfanyia Kila Kitu Ambacho Yeye Anaamini Kinakidhi Kwa Mwanamke Wake, Lakini Baada Ya ...Muda Mfupi Sana, Anaachwa! Anabaki Kujiuliza Maswali Yasiyo Na Majibu. Rafiki Yangu, Lazima Ujue Kwamba Pamoja Na Kuwa Mapenzi Hayana Kanuni Za Moja Kwa Moja, Zipo Ndogo Ndogo Ambazo Zikifuatwa, Mateso Kwako Yatakuwa Ni Kitendawili.
Huwezi Kukimbiwa Na Wanawake Bila Sababu Za Msingi, Lazima Kuna
Kitu Kinachosababisha Uachwe. Hapo Sasa Hakuna Sababu Moja, Wewe
Ukiachwa Kwa Sababu Hii, Mwingine Atakimbiwa Kwa Sababu Ile. Katika
Darasa Hili, Ukijifunza Kwa Umakini Utaweza Kujua Kasoro Yako Ilipokuwa
Na Kufanya Mabadiliko Ili ‘Usiachike’ Tena!
Wanaume Huwa Wanawalaumu Zaidi Wanawake Kutokana Na Sababu Za Hapa Na
Pale Zinazosababisha Kuachana Kwao. Lakini Wengine Hutoswa Bila Kuelezwa
Sababu Za Msingi, Akibaki Na Maswali Mengi Lakini Mwisho Hupata
Msichana Mwingine Kabla Ya Kuachana Naye Tena Bila Kujua Sababu
Halisi.Wakati Mwingine Sababu Zenyewe Huwa Za Maana Lakini Zingine Mh!
Ni Aibu Kuzitaja Hadharani. Hata Hivyo, Kuna Wengine Huamua Kuachana Na
Wapenzi Wao Kwa Makosa Ambayo Wao Hudhani Ni Makosa Kumbe Wao Ndiyo
Wanaokosea! Hebu Tuone…
JE UKOJE?Kama Una
Tatizo La Kuachana Na Wapenzi Kila Wakati, Kipegele Hiki Kinakuhusu!
Anza Kuangalia Tabia Zako Upya. Unaishije Na Mpenzi Wako, Jirani Zako Na
Watu Wanaokuzunguka? Unatumiaje Ulimi Wako? Wasichana Wengi Wanapenda
Wanaume Wachangamfu Na Wacheshi Wakiamini Kwa Namna Moja Ama Nyingine,
Ni Burudani Kwao Lakini Huwa Hawapendi Kabisa Uwachangamkie Wengine
Kupita Kiasi.Wanaume Wengi Hupingana Na Hili Lakini Utafiti Unaonyesha
Kwamba, Asilimia 70 Ya Wanaume Wanaowachangamkia Sana Wanawake, Mwisho
Wake Hufanya Nao Mapenzi Kama Siyo Kuingia Katika Uhusiano Moja Kwa
Moja. Usibishe, Tafiti Uone!Kama Una Tabia Hii, Hata Kama Unaamini
Kwamba Uchangamfu Wako Siyo Wa Nia Mbaya Kwa Wanawake, Achana Nao Maana
Unamkwaza Mpenzi Wako Bila Kujua. Wakati Mwingine Anaweza Kuonyesha Wivu
Lakini Mwingine Hawezi Kusema, Hivyo Hubaki Akiumia Moyoni Mwake Lakini
Akichoka Huamua Kuachana Na Wewe Hata Kama Anakupenda Akihofia Kuwa
Katika Penzi La Kuchangia. Angalia Vizuri Tabia Zako Katika Kipengele
Hiki.
MWANAMKE MATUNZO!
Hapa Jamani Inabidi Tuambiane Ukweli, Tena Bila Kufichana! Kuna Baadhi
Ya Wanaume Ni Wabahili Sana, Yaani Kutoa Fedha Kwa Wapenzi Wao Wanaona
Shida Sana. Visingizio Vya Kwamba Wao Siyo Mabuzi Ndiyo Vimewajaa
Akilini Mwao.Utawasikia Wakisema; “Mimi Siyo Buzi Bwana, Demu Wangu
Halafu Nimlipie? Haiwezekani!” Achana Na Hizo Fikra Ndugu Yangu.
Unatakiwa Utoe Matunzo Kwa Mpenzi Wako. Siyo Lazima Mpaka Akuambie! Ni
Jukumu Lako Kufahamu Aina Za Vipodozi Anavyotumia.Mnunulie Bila
Kukuambia, Mpelekee, Kuwa Mbunifu, Ukiona Nywele Zake Zinaanza Kufumuka,
Mpe Fedha Ya Saluni, Tena Ikiwezekana Mchagulie Mtindo Uupendao. Leo
Asuke Rasta Za Kimasai, Baada Ya Wiki Kadhaa Unambadilishia Mtindo
Mwingine.Jiulize Kama Wewe Ndiye Mpenzi Wake Halafu Unakataa Kumpa
Matunzo, Unataka Nani Amhudumie? Hivi Ulivyokutana Naye Akiwa Mzuri,
Anapendeza Unadhani Ni Nani Aliyekuwa Anamhudumia?Nakuhakikishia Ndugu
Yangu, Kama Huna Utamaduni Wa Kutoa Matunzo Kwa Mpenzi Wako Tarajia
Kukimbiwa! Kwa Maneno Mengine Ni Kwamba, Kama Hutoi Matunzo Kwa Mpenzi
Wako Ni Kama Umemruhusu Awe Katika Uhusiano Na Mwanaume Mwingine Ambaye
Atatoa Matunzo.Ni Wajibu Wako Kumnunulia Mavazi, Manukato Na Hata Fedha
Za Matumizi Yake Binafsi. Tatizo Hili Huwakumba Hata Wanandoa, Hawataki
Kuwahudumia Wake Zao, Wakidai Kwamba Wameshaoa! Usimpompendezesha
Atapendeza? Na Asipovutia Unadhani Nini Kitafuata Kama Siyo Kutafuta
Mwanaume Mwingine Nje? Upo Tayari Kusalitiwa?
Inawezekana Unashangaa Kwa Nini Wanawake Wanakukimbia Kila Siku, Kumbe
Kuna Sehemu Fulani Huwa Unakosea Bila Kujua. Hapa Ndipo Kwenye Dawa.
Ndiyo Sehemu Pekee Utakayoujua Ukweli Na Kuchukua Hatua.
Katika Sehemu Ya Kwanza, Wiki Iliyopita Nilianza Kwa Kuelezea Tabia
Mbili; Moja Ikiwa Kujiangalia Upya Tabia Zako Na Pili Ni Kumpa Matunzo
Mwenzi Wako.
Lazima Wanaume Mfahamu Kwamba Hata Gari Linapoharibika Huhitajika
Kupelekwa Gereji Kwa Kufanyiwa Ukarabati. Vivyo Hivyo Hata Mwanamke
Anahitajika Kupewa Matunzo Ili Aendelee Kuwa Bora Na Anayekuvutia.
Ukweli Ni Kwamba, Wanaume Wengi Hukwepa Kutoa Matunzo Ya Karibu Kwa
Wapenzi Wao Wakidai Wanachunwa! Nani Amekudanganya Ndugu Yangu? Kumtunza
Mpenzi Wako Siyo Kuchunwa!
Mpendezeshe Apendeze, Usipofanya Hivyo Wewe Unataka Nani Akutunzie? Kama
Una Tabia Hii Badilika Haraka, Maana Wanawake Wa Sasa Wapo Makini
Kuangalia Wanaume Ambao Wanatambua Wajibu Wao.
Kuna Mwingine Huwa Hatoi Fedha Mpaka Siku Atakayolala Na Mpenzi Wake,
Hiyo Ni Mbaya Zaidi Maana Hisia Za Kwamba Umemnunua Huanzia Hapo.
Najaribu Kuwaweka Sawa Na Kuwakumbusha Kwamba Mwanamke Anahitaji Matunzo
Na Kama Ukishindwa Kumtunza Utakuwa Unampa Mwanya Wa Kutafuta Mwanaume
Mwingine. Hapo Ndiyo Mwanzo Wa Usaliti.
UKOROFI, UKALI SI DAWA!
Watu Wanatambua Kwamba Mwanaume Ndiye Kichwa Cha Nyumba, Lakini Hilo
Lisiwe Kigezo Cha Wewe Kuwa Mkorofi Na Mjeuri Hata Kwa Mambo Mengine
Yasiyo Ya Msingi.
Mwanamke Anahitaji Mwanaume Mwenye Msimamo, Asiyeyumbishwa, Lakini Pia
Anatamani Sana Kusikilizwa Mawazo Yake. Mwanamke Anahitaji Kuliwazwa Na
Mpenzi Wake.
Ukali Kupindukia Hupunguza Mapenzi Na Hujenga Woga Na Hofu. Wakati
Mwingine Hushindwa Kukushirikisha Katika Mawazo Yake Mazuri Ambayo
Yangeweza Kujenga Kwa Kuhofia Ukali Wako.
Ni Vizuri Kuwa Makini Katika Hili, Huna Sababu Ya Kuwa Mkali Kwa Mpenzi
Wako. Mwanamke Ni Mtu Wa Kuelewa, Kama Kuna Mahali Amekosea, Zungumza
Naye Taratibu Huku Upendo Wa Kweli, Utii Na Utu Ukionekana Usoni Mwako
Na Hata Kinywani Mwako.
UMAPEPE
Kuna Baadhi Ya Wanaume Wana Tabia Ya Umapepe, Nikisema Hivyo Naamini
Naeleweka. Hili Ni Tatizo Lingine Wasilopenda Wanawake. Siyo Wanawake
Pekee Bali Hakuna Mtu Atakayejisikia Vizuri Mpenzi Wake Kuwa Na Tabia Ya
Umalaya. Kila Mmoja Anapenda Kuwa Na Penzi La Peke Yake Na Siyo La
Kuchangia!
Ikiwa Una Tabia Za Kupenda Kubadilisha Wanawake Kila Wakati, Tarajia
Kuachana Nao Kila Siku. Lazima Mwanaume Uwe Na Staha, Mapenzi Ya Kweli
Na Mtulivu Kwa Mwenzio.
Naomba Nieleweke Kitu Kimoja Hapa, Wakati Mwingine Hata Tabia Zako Za
Ajabu Ajabu, Zinamkosesha Raha Mpenzi Wako Na Fikra Za Kuachana Na Wewe
Zikizidi Kuusumbua Ubongo Wake.
Epuka Tabia Ya Kusifia Wanawake Wengine Vijiweni Au Ukiwa Na Mpenzi Wako
Katika Matembezi. Unapaswa Kujiheshimu. Heshima Unayoionesha Kwa Mpenzi
Wako Ni Kithibitisho Tosha Kwamba Unampenda Na Kuheshimu Uwepo Wake.
MPE KIPAUMBELE
Mwanamke Mwenye Mapenzi Ya Kweli Kwako, Lazima Atatamani Kujua Mambo
Mengi Kuhusu Wewe, Lakini Kubwa Zaidi Ni Uwazi Kuhusu Maisha Yake Pamoja
Na Kutoa Ushauri Kwako Pale Utakapohitajika.
Anapenda Kuona Ukimpa Nafasi Ya Kwanza Katika Maisha Yako, Uwe Wazi Kwa
Kila Kitu Kinachoendelea Katika Maisha Yako. Nafasi Ya Kwanza
Ninayoizungumzia Hapa Ni Pamoja Na Kuwa Naye Karibu Na Kumpa Taarifa Za
Mipango Yako Ijayo, Lakini Katika Hilo, Pia, Mwanamke Anapenda Kuona
Unaitambua Thamani Yake Na Kuyashika Maisha Yake Ipasavyo.
Mwanamke Akiona Hapewi Kipaumbele Na Mpenzi Wake, Hupoteza Imani Ya Kuwa
Na Mwanaume Huyo. Kama Una Tabia Hizi, Ndugu Yangu Achana Nazo,
Vinginevyo Kila Siku Utaishia Kubadilisha Wanawake Kama Nguo.
0 MAONI :
Post a Comment