Maafisa wa Kisiwa cha Malta wamesimamisha ndege
iliyotayarishwa kuwasafirisha wahamiaji haramu hadi Libya baada ya
Mahakama ya haki za binadamu ya Muungano wa Ulaya kuingilia kati.
Wiki jana wahamiaji 291 waliokolewa baada ya mtumbwi walimokua ndani kwenda mrama. Inaaminika mtumbwi huo uliwasili kutoka Libya na wahamiaji wengi wakiwa raia wa Eriterea.Katika msimu wa jua wahamiaji wengi wa Kiafrika huwasili katika visiwa vya Malta na Lampedusa wakijaribu kuingia Bara Ulaya.
Mahakama ya Ulaya ilitoa amri kusimamisha hatua ya kuwarejesha Afrika wahamiaji haramu waliokua Malta. Hii ilifuatia ombi la dharura kutoka kwa makundi ya kijamii.
Kamishina wa masuala ya ndani wa Muungano wa Ulaya Cecilia Malmstroem amesisitiza kwamba wahamiaji wa kiafrika wanaowasili katika maeneo ya Ulaya wana haki ya kuomba hifadhi.

0 MAONI :
Post a Comment