Tangaza na Abd Da Hustler

MWEZI WA RAMADHANI WAMBADILISHA WEMA


 
KUFUATIA Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au maarufu kama Madam amebadilika na kuondoa vitu vyote visivyo vya asili mwilini mwake.
 
Wema alitupia picha yake kwenye mtandao wa kijamii akionekana amekata nywele zote huku akiwa ameondoa kope za bandia na kutoa kucha alizobandika kuashiria kuuheshimu mwezi huu huku akibaki na kila kitu cha asili yake.
 
“Mwezi Mtukufu ni wa kuheshimiwa na kuweka kila kitu pembeni, nafurahi kuwa hivi kwa maana hata kama nikifunga swala zangu zitapokelewa vizuri,” alisema Wema
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment