Njama ya uasi pamoja na jaribio la wafungwa kutoroka
jela kubwa zaidi nchini Ivory Coast imetibuka na kusababisha vifo vya
wafungwa wawili.
Polisi walilazimika kurusha gesi ya kutoa
machozi pamoja na kufyatua risasi ili kutuliza hali katika gereza la
Maca mjini Abidjan.Maafisa wanasema kuwa walinzi wawili wa magereza walijeruhiwa vibaya.
Purukushani lilizuka Jumanne jioni wakati wafungwa kadhaa walipovunja milango ya magereza yao na kuwaachilia huru baadhi ya wafungwa.
Gereza hilo huwahifadhi wahalifu sugu na baadhi ya maafisa kutoka kwa iliyokuwa serikali ya rais wa zamani Laurent Gbagbo.

0 MAONI :
Post a Comment