Tangaza na Abd Da Hustler

Safari yakupa elimu


Sylvia na Mamake nje ya nyumba yao
Sylvia ni msichana wa miaka minane anaishi kijiji kimoja Tanzania, licha ya maisha yake amejitolea kupata elimu na kila siku hutembea kwa saa moja unusu kwenda shuleni. Yeye ni miongoni mwa wasichana waliobahatika kupata elimu Barani Afrika

Nyumba ya akina Sylvia na shamba lao 
 
Mamake Sylvia aliolewa tena baada ya mumewe wa kwanza na babake Sylvia kufariki dunia. Familia 
hii inaishi kilomita 300 kutoka Jiji Kuu Dar Es Salaam. 
 
Msichana wa Tanzania akipitia kichakani
Shule ya Sylvia iko kilomita saba na msichana huku hutembea kila siku akipitia kichakani,wakati mwingine anaumia miguu, pia lazima aepuke kukanyanga wanyama hatari kama nyoka.

Sylvia akielekea shuleni anapitia njia tofauti
Mtoto huyu hupitia njia nyingi familia yake ni masikini na haiwezi kumnunulia viatu. Japo hakuna karo anayolipiwa, imekua vigumu kwa wazazi wake kununua vitabu au sare za Sylvia za shule.
Lori hili lampita Sylvia akielekea shuleni
 Safari ya msichana huyu kisha inampeleka barabara kuu. Wakati mwingine kuna jua kali, vumbi nyingi. Msimu wa jua barabara hujaa mapote na inampa changamoto msichana huyu katika safari yake shuleni
Sylvia akitumia njia ya reli kuelekea shuleni
 Ikiwa msichana huyu hataki vumbi na matope ya barabara, huamua kupitia kwenye njia ya reli. Hata hivyo kuna hatari zake, treni huenda ikaamkanyanga. Wakati mwingine watoto wa shule wamekua wakitekwa nyara.
Sylvia akipitia  kichochoro kueleka shuleni
 Kuna vichochoro vingine kando ya barabara kuu ambavyo Sylvia hutumia, lakini kuna hatari ya kukumbana na wabakaji.
Sylvia akielekea kuingia shuleni
Baada ya pita pita hizo hatimae Sylvia huwasili shuleni.Msichana huyu anasema ataendelea na elimu yake licha ya safari ndefu ambayo hufanya kila siku.

Sylvia na rafiki yake Radhia
                          Sylvia ana rafiki Radhia ambaye huandamana naye kuelekea shuleni pamoja.
Sylvia anaelekea darasani
Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na Utawaduni-UNESCO asili mia 62 ya wasichana Afrika wameweza kuingia shule za upili, hata hivyo nchini Tanzania ni asili mia 32 pekee ya wasichana ambao wanaweza kujiunga na shule za upili.
Sylvia na familia yake
BBaba wa kambo wa Sylvia amekua akiona malezi yake kama mzigo hasa elimu, lakini kwake Sylvia anasema elimu ni njia pekee ya kubadilisha maisha ya familia yake.
                 
                                                                        MWISHO;
 
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment