Tangaza na Abd Da Hustler

TAARIFA YA YANGA KUHUSU MKATABA WA AZAM MEDIA NA KAMATI YA LIGI/TFF.




















mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji (katikati) akiongea na waanidishi wa habari, Makamu mwenyekiti Clement Sanga (kushoto) na mjumbe wa kamati ya utendaji Mark Anthony (kulia)












Uongozi wa klabu ya Yanga leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu ya urushwaji wa michezo yake ya Ligi Kuu katika kituo cha luninga cha Azam ambacho kimeingia makubaliano na kamati ya Ligi Kuu  kuonyeshwa michezo yote ya ligi kwa kipindi cha miaka miatatu (3).
Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji amesema uamuzi wa kamati ya ligi kuingia mkataba na kituo cha Azam Tv bila ya kuwashirikisha wahusika wenyewe ambao ni vilabu vishiriki haukuwa sawa.
Sisi kama klabu ya Yanga tulikaa kikao cha kamati ya utendaji na kuona taratibu za kupewa haki ya matangazo kwa kampuni ya Azam haikua sawa, sisi viongozi wa kalbu ya Yanga hatukushirikishwa katika mchakato huo hivyo tukaona ni vema tuje kwa vyombo vya habari tuulezee umma juu ya maazimio ya kamati ya utendaji.
Ifuatayo ni taarifa kamili kwa vyombo vya habari: 
YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.

Hivi karibuni, Tanzania Football Federation (TFF)  iliunda Tanzania Premier League chini ya Bodi ya mpito Bodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina  mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:

1. BODI YA TPL

1.1 Bodi iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe  ……….. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.

1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.

1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.

2. UTARATIBU WA DUNIA NZIMA

2.1 Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani. 

2.2 Mfumo (undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa YANGA iachie  urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya Tanzania.

2.3 Makubalianokati ya TPL na Azam Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA na Klabu zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania  watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.

2.4 Kamati ya Utendaji ya YANGA siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi, lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa: 

2.4.1 Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa washabiki wengi; 

2.4.2 Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na Wanachama; 

2.4.3 Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.

3. MIGOGORO YA MASLAHI

3.1 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa Makampuni ya Azam na  kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL na Azam ni ya kutiliwa mashaka.

3.2 Makampuni ya Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji wa vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu zaidi kuliko mprira  wa miguu, kama vile Azam F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya mpira wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa YANGA.

3.3 Azam na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.

4. KUTOKUWA NA UWAZI

4.1 Mkataba wa utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya habari,  na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za kurusha matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania Premier League).

4.2 Ukosefu wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya ombi hilo kwaTPL.

5. MAZINGATIO YA KIBIASHARA 

5.1 Mamlaka ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA. TPL inasingizia  kwamba leseni ya matangazo ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa kuukubali "lock, stock and barrel."

5.2 TPL inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji  wa mchezo ya mpira inayotarajia kuingia na Television ya Azam kama "makubaliano ya udhamini" (“sponsorship agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara inayotokana na maslahi ya uhusiano na hivyo 
wahusika wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.

Kwa mfano, moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA  Dar es Salaam huingiza makusanyo ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25% katika mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya mapato takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa, wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji)  walikuwa wanaafikiana kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.

Kamati ya Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.

Msisitizo wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.
......................
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
29 JULAI, 2013
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment