Tangaza na Abd Da Hustler

Kiongozi mkuu wa Al Shabaab ajisalimisha

                                                   Kiongozi wa alshabaab Dahir Aweyes
Umoja wa mataifa unasema kuwa kiongozi mmoja mkuu wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia, al-Shabab, Hassan Dahir Aweyes, amejisalimisha kwa wanajeshi wa Somalia.
Bwana Aweyes alitafuta hifadhi mjini Adado,mji ulio umbali wa kilomita miatano kaskazini mwa Mogadishu baada ya mapigano makali kati ya mirengo ya Al Shabaab mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa kiukoo, wamekwenda huko kujadili watakachofanya naye baada ya kujisalimisha kwake.
Lakini viongozi hao wamefahamisha mwandishi wa BBC kuwa amekanusha madai kuwa amejisalimisha na kwamba amekataa kusafiri kwenda Mogadishu.
Bwana Aweyes amekuwa akijulikana kama kiongozi mkubwa katika kundi la al-Shabab na Umoja wa mataifa na Marekani zinamfahamu kama gaid
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment