Vikosi vya usalama vinaendelea
na juhudi za kukabiliana na magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya
huku mateka wakinusuriwa. Katika ukurasa huu tutakupasha moja kwa moja
matukio yanavyojiri katika jengo la Westgate ambako inaarifiwa vikosi
vya usalama vimezingira jengo hilo na hata kudhibiti sehemu ya jengo
zima. Ikiwa uko karibu na uwanja huo unaweza kutupasha hali unavyoona
kupitia kwa ukurasa wa https://www.facebook.com/abddahustler?ref=hl
14:28 Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema kuwa moshi ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi wlaioko ndani ya jengo hilo kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi yao
14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama vinakaribia kudhibiti hali na vimeingia ndani kabisa ya jengo hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka
14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo
13:54: Mwandishi wa BBCIdriss Situmaaliye katika eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo
13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili kuwawezesha kufanya kazi yao
Waathirwa wa shambulizi la Westgate
13:19 pm Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika jengo la Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka wakenya ambao idadi yao haijulikani
13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab
12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya jitahada za misho kuwa

0 MAONI :
Post a Comment