Tangaza na Abd Da Hustler

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry akisema kuwa Marekani imetoa msaada kwa serikali ya Kenya ili kuweza kupambana na hali hiyo

Vikosi vya usalama vinaendelea kukabiliana na wavamizi wenye bunduki ambao wamewaua watu 39 na kuwajeruhi wengine 150 katika shambulizi lililofanywa katika jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi, ambako wanamgambo wa alShabaab wanawashikilia mateka idadi isiyojulikana ya watu. Kundi la al-Shabaab nchini Somalia limedai kufanya shambulizi hilo. Ufaransa imesema raia wake wawili wameuawa, huku pia Canada ikisema imewapoteza raia wake wawili ikiwa ni pamoja na mwanadiplomasia mmoja. Rais wa Kenya uhuru Kenyatta amesema maafisa wa usalama bado wanafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa wanaokoa maisha ya watu wanaoaminika  kuwa  wanashikiliwa mateka ndani ya jumba hilo. Amelaani shambulio hilo akisema serikali itafanya kila iwezalo kuwakamata wahalifu hao. Kundi la al-Shabaab lilikuwa limetoa vitisho vya kuishambulia Kenya, kama hatua ya kulipiza kisasi uvamizi uliofanywa na jeshi la Kenya nchini Somalia. Marekani pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio hilo, huku Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry akisema kuwa Marekani imetoa msaada kwa serikali ya Kenya ili kuweza kupambana na hali hiyo.

Washambuliaji wa kundi la kigaidi la Al Shabaab walivamia jengo hilo

 
 Wanawake, watoto na watu wazima huzuru jengo hilo mwishoni mwa wiki kujivinjari na ni hao hao waliojikuta katika hali ya mguu niponye

 
Hali ilikuwa mbaya kwani washambuliaji waliwapiga risasi kiholela wakenya waliokuwa ndani ya jengo hilo na hawa wanaonekana kukimbilia usalama wao

 
Polisi waliweza kufika mara moja katika eneo la shambulio kukabiliana na wapiganaji ambao idadi yao kamili haijaweza kusemwa

 
Baada ya masaa tano ya taharuki ndani ya jengo hilo milio ya risasi ilikuwa inasikika ishara ya makabiliano kati ya polisi na wanamgambo hao
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment