
Sala Uddin Quader Chowdhry
Kiongozi wa ngazi ya juu wa Upinzani wa chama cha Bangladesh Nationalist Party, BNP, amehukumiwa adhabu ya kifo hii leo kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wakati wa vita vya kudai uhuru kutoka Pakitan mwaka 1971. Sala Uddin Quader Chowdhry amehukumiwa katika mahakama maalum inayochunguza madai dhidi ya wanasiasa wanaoshukiwa walishirikiana na vikosi vya Pakistan katika vita hivyo vilivyodumu miezi tisa. Chowdhry ni mbunge mwenye umri wa miaka 64 na amekutikana na hatia ya kushiriki kufanya mauaji ya halaiki, utekaji nyara na mateso wakati huo wa vita vilivyosababisha kiasi watu milioni 3 kuuwawa na wanawake 200,000 walibakwa wakati maelfu ya makaazi yaliteteketezwa. Jaji Fazle Kabir aliyeongoza jopo na majaji watatu katika kesi hiyo ametoa hukumu hiyo leo kukiwa na ulinzi mkali wa vikosi vya usalama katika mahakama hiyo.
0 MAONI :
Post a Comment