1.Utafiti
uliofanywa barani ulaya umegundua kuwa wanafunzi ambao ni mashabiki wa
mchezo wa soka hufanya vibaya kwenye mitihani yao wakati timu zao
zinapofanya vizuri yaani timu inaposhinda takwimu za matokeo ya mitihani
huwa chini. 2.Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na The Happy Planet Index
nchi inayoongoza kwa furaha duniani ni Costa Rica,marekani inashika
nafasi ya 105 kwenye orodha ya nchi zenye furaha duniani.
San Jose Costa Rica
3.Kuna kitabu kimoja ambacho kinaitwa “what every man thinks
about apart from sex” yaani “kitu ambacho wanaume wanafikiria tofauti na
ngono”. kitabu hiki kimewahi kuweka rekodi ya mauzo ya juu , cha
kushangaza kuhusu kitabu hiki ni kwamba kina kurasa 200 ambazo
hazijaandikwa kitu chochote ndani yake. 4.Nchi
ya marekani ni nchi ambayo inaongoza kwa kuwa na sheria za ajabu ,
mojawapo ya sheria hizo ni sheria iliyowekwa na serikali ya jimbo la
North Carolina ambayo inasema kuwa ni hatia kuimba off key yaani ukiimba
nje ya zile key za muziki basi umefanya hatia na unaweza kutozwa faini
au kutumikia kifungo gerezani.
0 MAONI :
Post a Comment