Ghorofa tatu za jengo la Westgate ziliporomoka
Maafisa wa ujasusi nchini Kenya
wanaochunguza shambulizi la kigaidi lililotokea mwezi jana katika jengo
la Westgate, wanasema dalili zinaonyesha kuwa huenda waliofanya
mashambulizi hayo ni wanachama wa mtandao wa kigaidi nchini Kenya
Mwandishi wa BBC anasema kuwa madai ya awali kuwa magaidi hao walitoka nje ya Kenya yanaonekana kutokuwa na msingi.Pia kuna ripoti za wanajeshi kupora maduka yaliyokuwa ndani ya jengo hilo. Watu 67 waliuawa na wengine zaidi ya miamoja sabini kujeruhiwa. Hadi sasa watu 39 hawajulikani waliko.
Kundi la kigaidi la Al-Shabab limekiri kutekeleza mashambulizi hayo.
Madai ya awali ya maafisa wa ujasusi kuwa wanamgambo wenye uraia wa uingereza walikuwa miongoni mwa wavamizi hayajapatikana kuwa na msingi.
Kuna ushahidi kuwa wanamgambo wa kisomali wa Al Shabab wamevuka mipaka na kuingia nchini humo kwa shughuli ya kuwasajili wapiganaji vijana kwa lengo la kuwapa mafunzo ya kigaidi.
0 MAONI :
Post a Comment