Maelfu ya watu wanakimbilia usalama wao kutokana na vita kutokota Sudan Kusini
Ripoti kutoka Sudan Kusini
zinasema kuwa wanajeshi walio watiifu kwa serikali ya rais Salva Kiir
wanaendelea kuukaribia mji wa Bentiu unaodhibitiwa na waasi katika eneo
lenye utajiri wa mafuta Kaskazini mwa taifa hilo.
Mwandishi wa BBC aliye mjini Bentiu anasema
wanajeshi wa serikali wanaaminika kuwa umbali wa kilomita ishirini na
tano kutoka mji huo na raia wameingiwa na hofu kubwa.Maelfu ya watu wanaripotiwa kukimbilia kwenye makao ya jeshi la kulinda amani ya umoja wa mataifa katika mji huo.
Wanajeshi wanaomtii aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar wameripotiwa kuanza kujiondoa katika eneo la makabiliano.
Mapigano yaliyozuka kote nchini Sudan kusini mwezi uliopita na ni mafanikio kidogo yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kumaliza ghasia hizo
0 MAONI :
Post a Comment