Lionel Andrés Messi mwishoni mwa mwaka 2013 alitua Tanzania kimya kimya
kufanya tangazo la Turkish Airlines kwenye Mlima Kilimanjaro? Ni ngumu
kuthibitisha hilo lakini kwa mujibu wa tangazo hilo, Messi anaonekana
akijipiga picha juu ya Mlima huo mrefu barani Afrika.
Idea ya tangazo hilo ni kuwa Messi na mchezaji wa mpira wa kikapu wa
timu ya Los Angeles Lakers, Kobe Bryant wanashindana kupiga picha bora
zaidi aina ya selfie. Tangazo linaanza kwa Messi kumtumia picha Kobe
yake mwenyewe akiwa mbele ya kanisa la Saint Basil’s Cathedral mjini
Moscow.
Kobe naye anajibu mapigo kwa kwenda kwenye kuta maarufu za China (The
Great Wall of China) na mashindano yanaendelea hadi kumfanya Messi aje
kuchukua selfie kwenye mlima Kilimanjaro, huku maeneo yote hayo
yakifikika na ndege za Turkish Airlines. Mwisho Messi anajipiga picha
akiwa Sultanahmet Square mjini Istanbul, na kuja kugunduaa nyuma yake
alikuwepo Kobe aliyetokea pia kwenye picha yake.
Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
0 MAONI :
Post a Comment