Tangaza na Abd Da Hustler

[Sports; Tennis] Stanislas Wa Uswisi Ndiye Bingwa Mpya Wa Australian Open

STANISLAS
Japo hakutegemea kufika hapa, Stanislas Wawrinka, 28 kutoka Uswisi amefanikiwa kutwaa ubingwa huu mpya wa mashindano ya Tennis yanayojulikana kama Australian Open baada ya kumshinda Rafael Nadal, mkali kutoka Hispania kwa seti tatu kwa moja kwa matokeo ya 6-3  6-2  3-6  6-3. Japo Nadal alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo, lakini maumivu hayo hayakumzuia kuingia ulingoni kupambana na “Stanimal”
Anakuwa raia wa pili wa Uswisi kunyakua taji hilo la Grand Slam kwa upande wa wanaume kwa mchezo wa tenesi na mchezaji mmoja mmoja.
Naye Wawrinka alimsifu Nadal kwa kuwa bingwa wa kweli na kinara wa kweli wa tenesi duniani kwa wanaume, alikiri hujisikia furaha kupambana na kumshinda bingwa kama Nadal.
Wawrinka hajawahi kushinda hata seti moja katika michezo yote 12 aliyokutana na Nadal huko nyuma, na alicheza fainal yake ya kwanza akiwa kwenye nafasi ya 19 ya ubora wa tenesi duniani.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment