Tangaza na Abd Da Hustler

Chukua hiyo: Chief Kiumbe ni mtaalamu wa Kung Fu, Karate, Kick Boxing na kucheza na panga kama Ninja, Msikilize hapa

Pichani: Chief Kiumbe (kulia) akiwa na Diamond.
Kama wewe uliwahi kuwa na ulevi kama wangu wa kuangalia filamu za karate na kung fu za wachina hususani enzi hizo, utakuwa umeona mara kadhaa kwenye filamu hizo kijana mbabe wa mtaa wao, aliyemchukulia poa mzee fulani na kumzingua mwisho anapokea kichapo kikali kutoka kwa mzee huyo.
Hii inaweza kuwa hivyo kama ukimchukulia poa mfanyabiashara maarufu hapa Tanzania anayejulikana sana kupitia wasanii mbalimbali wanaomtaja kwenye hits zao, Mohamed Abdallah Kiumbe aka Chief Kiumbe.
Nakupa hii, Chief Kiumbe ambaye ni mzaliwa wa Musoma, Mara aliwahi kutikisa sana miaka ya 90 Tanzania kwa mchezo wa Karate na Kick Boxer, huku akifanya maonesho kadhaa na kuonesha uwezo wake wa kucheza na panga kama Ninja.
Binafsi niliwahi kushuhudia moja kati ya maonesho yake akiwa na mtaalam mwingine ambaye ndiye aliyekuwa mwalimu wao akifahamika kwa jina la Abdallah Kuncha. Enzi hizo Chief Kiumbe alikuwa anajulikana kwa jina lake halisi, Abdallah Kiumbe.
Enzi hizo wababe wa mji huo na wakali wa karate walikuwa wanahesabika akiwemo kaka yake Chie Kiumbe anayejulikana kwa jina la ‘Rambo’, hadi leo ni mzee wa makamo anaeogopwa sana kwa uwezo wake katika mchezo huo.
Chief Kiumbe mwenyewe alifunguka na kuweka wazi kuhusu utaalam alionao katika mchezo huo wa mapigano, kupitia kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm kinachoongozwa na Samira, Fadhili Haule, Fredwaa na Erick Martin.
“Musoma, baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika ile hospitali ya Musoma, nadhani kila baada ya miaka mitano huwa wanakuja wachina katika hiyo hospitali. Kwa hiyo before…miaka ya nyuma tulipokuwa tunasoma, walikuwa wanatufundisha karate na niliupenda sana huo mchezo kwa sababu kuna kaka yangu mkubwa alikuwa anaufanya. Kwa hiyo sisi katika familia yetu kuna watu wawili tu ambao hawakuucheza.” Alifunguka Chief Kiumbe.
Chief Kiumbe, alicheza michezo mikali inayojulikana kwenye ulimwengu wa mapigano ya kutumia ufundi.
“Nilicheza Kung-fu ambayo tulifundishwa na wachina, baadae nikacheza Kick Boxer, nilifundishwa na rafiki yangu Gamba akiwa Morogoro. Na baada ya hapo nilicheza Karate niliyofundishwa na Kuncha.” Alieleza Chief Kiumbe.
Ukiacha Michael Dudikoff aliyetamba na filamu ya ‘American Ninja’, Chief Kiumbe na familia yake ni kati ya waanzilishi wa ‘American Ninja ya kibongo’.
“Sisi ndio waanzilishi wa ile American Ninja (Tanzania), zamani sana tulikuwa tunacheza na mapanga. Kwa hiyo ni self-defence.” Anakaririwa Chief Kiumbe.
Najua swali la msingi litakuwa, je, leo hii huyu Chief unaemfahamu bado anayaweza mapigano? Ujuzi hauzeeki.
“Hiyo haiwezi kutoka damuni, japokuwa mwili upo…lakini ukinipa kwa dakika tatu, dakika tatu shughuli yangu ataiona. Akinipitisha hapo na mimi naweza kuiona shughuli yake, lakini ile haitoki damuni..ipo.” Amejigamba mkali huyo wa mapigano.
Endelea kufuatilia hapa, siku moja tutakuelezea kwa undani kuhusu Chief Kiumbe na siri ya utajiri wake.
Msikilize hapa:
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment