Tangaza na Abd Da Hustler

Jaguar aendelea kupepea, asaini mkataba na kampuni ya MTech itakayosambaza kazi zake Afrika


Msanii anayedaiwa kuwa na utajiri mkubwa kuliko wasanii wengine nchini Kenya, Jaguar anazidi kupanda ngazi za mafanikio kupitia muziki wake baada ya kusaini deal nono na kampuni ya MTech Kenya itakayokuwa na jukumu la kusambaza kazi zake Afrika.
Menejimenti ya Jaguar, imeiambia Red Pepper Online kuwa msanii huyo alikuwa anaangalia katika kutanua fan base yake Afrika Magharibi na Kusini na kwamba MTech ambao wanapatikana huko na wanaushawishi walikuwa watu sahihi wa kufanya nao kazi kwa kuzingatia lengo lake.
Baada ya kusaini mkataba huo na MTech, Jaguar anatarajiwa kuingia studio kufanya kazi na rapper wa Naija ‘Ice Prince’ ambaye alishinda tuzo ya BET.
Jaguar anaungana na  P-Unit, Wyre, Radio & Weasel, Keko wa Uganda, Victoria Kimani, Ice Prince, P Square, Flavour, J Martins, Brackets Eko Dida na wengine ambao wanafanya kazi na MTech.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment