Afisa mwandamizi wa shirika la
kutetea haki za kibinaadamu ameiambia BBC kwamba baada ya siku au
majuma machache Waislamu wote wataihama Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mkurugenzi wa maafa wa Shirika la Kutetea haki
za kibinaadamu, Human Rights Watch, Peter Bouckaert, amesema matokeo
hayo yatakuwa mabaya kwa uchumi wa nchi kwa sababu Waislamu wanadhibiti
soko la nyama na biashara kadha.Bwana Bouckaert amesema watu tisa wameuwawa katika mji mkuu, Bangui, na Jumapili aliona Muislamu akipigwa mapanga hadi kufa.
0 MAONI :
Post a Comment