Kanye West Jukwaani anasesemekana kuwa na tatizo la kudhibiti hasira
Mwanamuziki wa muziki wa kufoka
au Rap nchini Marekani Kanye West, hajakana wala kukubali mashitaka ya
kumshambulia mpiga picha katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Los
Angeles.
Adhabu yake ni kifungo cha nje cha miaka miwili
na ameshurutishwa na mahakama kupata ushauri nasaha kuhusu anavyoweza
kudhibiti hasira. Pia ametakuwa kuhudumia jamii kwa masaa 250 kwa kosa
hilo alilofanya Julai mwaka jana.Muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 36 anasisitiza kuwa hana hatia.
Daniel Ramos
"nilikuwa nafanya kazi yangu wakati West aliponishambulia, '' alisema mpiga picha huyo, '' ikiwa ni mimi ningekuwa nimemfanyia kitendo hicho ningekuwa kizimbani.''
Ramos pia alidai kuwa alihofia kulipiza kisasi baada ya matamshi ya muimbaji huyo kupitia kwenye televisheini.
West alikamatwa mwaka 2008 kufuatia vurumai lengine na mpiga picha katika uwanja huohuo wa ndege.
Kesi hiyo, ilitupiliwa mbali na mahakama baada ya West kuwalipia vifaa vilivyoharibika na pia kupata ushauri nasaha kuhusu namna ya kudhibiti hasira zake.
0 MAONI :
Post a Comment