Tangaza na Abd Da Hustler

Video: Mhindi atayarisha filamu ya Ndege ya Malaysia iliyopotea, aiita 'Vanishing Act' angalia trailer yake hapa

Wakati bado dunia imeshindwa kufahamu mahali ilipo ndege ya Malaysia (Flight MH370) iliyopotea huku ndugu na jamaa wakiwa na majonzi ya kutojua hatma ya wapendwa wao, mtayarishaji Rupesh Paul yeye ameamua kutayarisha filamu inayohusu tukio hilo. Rupesh Paul ambaye ni raia wa India tayari ameanza kutayarisha filamu hiyo huku watu wakiwa hawafahamu hata nini chanzo hasa cha kupotea kwa ndege hiyo na matukio yaliyojiri ndani ya ndege.
Mtayarishaji ameiambia Hollywood Reporter kuwa filamu hiyo haitaumiza hisia za ndugu na jamaa za abiria waliopotea na ndege hiyo na kwamba hakuna matumizi yoyote ya bunduki yatakayooneshwa.

“Haitahusu vitu vya kijinga. Hakutakuwa na matumizi ya bunduki na hakutakuwa na matumizi mabaya ya vitu vya kigeni.” Alisema Rupesh Paul.
Katika kutetea uamuzi wake wa kutumia tukio hilo kama sehemu ya filamu yake, alieleza kuwa haoni umuhimu wa kutengeneza filamu ambayo haiwavutii watu.
“Watu hawataki Makala, wanataka kitu kitakachowasisimua. Kwa nini nitayarishe filamu kuhusu kitu kingine chochote ambacho hakiwavutii watu?” Alihoji. 
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment