Watu
watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliohusika na utekaji na
unyan'ganyi wa gari Mei 12 mwaka huu eneo la Mlima Msangamwelu Wilaya ya
Mbeya Vijini wameuawa na wananchi katika mapambano makali pembezoni mwa
Mlima Mbeya.
Jambazi
la kwanza lilitambuliwa kwa jina la Kitwana Lugoya(30)mkazi wa Ilemi
Juhudi Jijini Mbeya ambaye aliuwa na wananchi baada ya kupata taarifa
ambapo walifanikwa kumzingira na kufanikiwa kumkamata eneo la
Msangamwelu Kata ya Mshewe.
Juhudi
za wananchi ziliendelea kwa kushirikiana na Jeshi la kuwasaka majambazi
wengine ziliendelea na kufanikiwa kuwakamata majambazi wengine wawili
waliotambuliwa kwa majina ya Ndayobi Lutego(26)mkazi wa Igunga mkoani
Tabora na Idd Sadiki(29) mkazi wa Veta Jijini Mbeya.
Hata
hivyo juhudi za wananchi ziliendelea kuwasaka majambazi wengine wawili
waliosalia wakiwa na bunduki na risasi kadhaa ambao walitokomea katika
msitu mnene kupandisha Mlima Mbeya na kufanikiwa kukamata jambazi
jingine lililokuwa na silaha na mfuko wa risasi ambapo wananchi
walilidhibiti ndipo alirusha silaha na risasi msituni na kuanza
kupambana na wananchi kwa kusaidiana na Askari na kufanikiwa kumkamata
na katika mapambano hayo jambazi hilo liliuawa kwa kutumia silaha za
jadi na mawe.
Jambazi
mwingine alikamatiwa katika Kitongoji cha Lunji Kijiji cha Ihombe kwa
ushirikiano na wananchi wa vijiji vya Ihombe,Iziwa,Ikukwa na Msangamwelu
ambalo pia lilipambana na wananchi hao na Askari majira ya saa tano
asubuhi Mei 13 mwaka huu ambapo lildhibitiwa na kuuawa.
Mapambano
hayo ya hatari katika msitu huo yalikuwa yakifanyika kwa tahadhari
kubwa kutokana na kutojua idadi yao na aina ya silaha walizo nazo na
mpaka sasa silaha na risasi havijapatikana katika msitu huo.
Baadhi
ya majambazi kabla ya kuuawa imedaiwa kujihusisha na matukio ya
ujambazi wa kutumia silaha katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo
Njombe,Iringa na Morogoro ambapo walikuwa wakitafutwa kwa muda mrefu na
Jeshi la Polisi.
Jeshi
la Polisi limewashukuru wananchi waliojitolea kupambana na majambazi
hao kwa kutumia dhana ya Polisi Jamii na ulinzi shirikishi ambayo
imeanza kuzaa matunda na kufanikiwa kukomesha vitendo vya uhalifu Mkoani
Mbeya ili Mbeya iwe na amani muda wote.
Wakati
wa uporaji majambazi hayo yapatayo matano yalipanga mawe barabarani
eneo la Msangamwelu na kufanikiwa kupora pesa,simu na pikipiki aina ya
SANYA yenye namba T 682 CHT ambayo baadaye waliitelekeza msituni
walipokuwa wanafuatiliwa na wananchi.
Majambazi
hao walimjeruhi Dereva wa roli hilo aliyefahamika kwa jina la Sephen
Mgogo ambaye amelazwa katika Hospitali Teule ya Ifisi na miili ya
majambazi hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya ambapo
wawili kati yao hawajatambuliwa.
Jeshi
la Polisi waliondoka Kijiji cha Ihombe majira ya saa moja na nusu usiku
baada kazi ngumu ya kubeba miili ya majambazi hao mwendo wa masaa
matano kwa miguu kutoka uneo la mapambano.
|
0 MAONI :
Post a Comment