Tangaza na Abd Da Hustler

BAADA YA SULUHU NA HONDURAS, GERRARD AMJIA JUU MWAMUZI WA MTANANGE HUO

NAHODHA wa England, Steven Gerrard amesikitishwa na kiwango kibovu cha mwamuzi katika suluhu waliyoipata jana dhidi ya Honduras ikiwa ni mechi ya kulipashia kombe la dunia mjini Miami.
Pia Gerrard amewalaumu wapinzani wao kwa mchezo mbovu ambapo wachezaji wanne walioneshwa kadi za njano na Brayan Beckeles alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Leighton Baines na hii ilitokana na kupata kadi mbili za njano.
Hata hivyo mechi hiyo ilisimama kwa nusu saa kutokana na umeme kukatika uwanjani, lakini haikupunguza kasi ya Honduras walioonesha kuwa hatari katika mechi hiyo.
Unhappy: England captain Steven Gerrard criticised the refereeing after England's draw with Honduras
 Gerrard amemkosa mwamuzi Salazar na wachezaji wa Honduras baada ya mechi.
“Tulikuwa na mawazo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo”, aliwaambia waandishi wa habari. “Tulifikiri kuwa mwamuzi alikuwa mbovu. Lakini tumefurahi kwasababu hatujapa majeruhi yeyote”.
“Walikuwa wanacheza vibaya wakati wanajua imebaki wiki tu kuanza kombe la dunia. Nashangaa sana inapotokea mchezaji anacheza mpira kifuani kwa mchezaji, ile ni kadi nyekundu. Ilitokea kipindi cha kwanza na pengine ingebadili mpira”.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment