Tangaza na Abd Da Hustler

Majeshi ya Marekani kwenda Iraq tena?

Rais Obama amesema anaangalia uwezekano wa kuisaidia Iraq kukabiliana na mashambulizi ya wanamgambo wa kiislam waonadhibiti eneo kubwa la kaskazini mwa Iraq .
Hata hivyo maafisa wa Marekani wamesema wanaendelea na majadiliano ili kuona kama wanaweza kutuma vikosi vya kijeshi katika kukabiliana na kundi hilo.
Nchini Iraq kwenyewe wanamgambo hao wamepata udhibiti zaidi mashariki mwa jimbo la Diyala, lakini mashambulizi ya anga ya vikosi vya serikali yameelekezwa magharibi zaidi eneo la Samara.
Katibu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema hali hiyo haivumiliki juu ya vitendo dhidi ya wanamgambo hao wa kiislam japo kuwa Iraq yenyewe inapaswa kutafuta namna ya kutatua mgogoro huo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jen Psaki ametoa ufafanuzi akidai kuwa watalaam wao bado wanaendelea na majadiliano na kwamba si nia ya nchi yake kurejesha vikosi vyake Iraq japo kuwa inaona haja ya kutoa msaada kwa nchi hiyo kutokomeza makundi hayo.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment