Wanajeshi wa Thailand
Kiongozi wa jeshi nchini
Thailand ametangaza bunge jipya ambapo wanajeshi wengi watachukua viti
vingi litapobuniwa katika kipindi cha miezi miwili ijayo pamoja na
serikali ya mpito.
katika hotuba yake kwa taifa kupitia runinga ya
taifa hilo Jenerali Prayuth Chan Ocha pia amesema kuwa katiba mpya
itaandikwa katika kipindi cha mwaka mmoja ujao huku uchaguzi ukifanyika
miezi mitatu baadaye.Mwandishi wa BBC mjini Bangkok anasema kuwa Jenerali Prayuth aliweka wazi kwamba jeshi litashikilia mamlaka hadi wakati huo.
kumekuwa na shutma za kimataifa kuhusu mpango wa jeshi hilo kuimarisha demokrasia nchini humo baada ya kuipindua serikali mwezi uliopita.
0 MAONI :
Post a Comment