Tangaza na Abd Da Hustler

U15 Tanzania Yatua kutua leo Tanzania na Medali Vifuani

Timu ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 15 iliyoshika nafasi ya pili katika Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) iliyofanyika Gaborone, Botswana inawasili leo (Juni 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
U15 ambayo imeshinda mechi tatu, sare moja na kufungwa moja inawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Gaborone kupitia Nairobi.
Tanzania ambayo imepata medali za fedha kwa kushika nafasi hiyo ikiwa chini yaKocha Abel Mtweve ilizifunga Afrika Kusini 2-0, Botswana 2-0, Swaziland 3-0 na ikatoka sare ya bao 1-1 na Mali. Ilifungwa mabao 2-0 na Nigeria ambao ndiyo walioibuka mabingwa.
Wachezaji 16 waliounda kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindek
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment