Tangaza na Abd Da Hustler

Balozi wa Libya Tanzania ajiua


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo imepokea taarifa kutoka Ubalozi wa Libya hapa nchini kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya, Bwana Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi. Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa Saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Lbya. Inataarifiwa kuwa Bwana Nwairat alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto. Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini. Walimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay ambako alitangazwa kuwa alikwisha kufariki na Polisi walithibitisha kifo hicho. Maiti imehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha…
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment