![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgXvCGnUAbqpp7r2-HR9sXubKKtGJS1SgknSXROFyWXfjUvMFfN3NIruXIfI2h9p6dGcMptL5Z4yCJuXuJSbERDEuLifL1MacWC5thx2Jf3zDgmjPY-OdPJx_GXnd3TnSFTojnBoEOnBFE/s640/141106221249_sp_osama_bin_laden_promo_640x360_reuters.jpg)
Osama Bin Laden
Kundi la kigaidi la A Qaeda limetoa ujumbe wa sauti ambao unadai kwamba umetoka kwa Hamza Bin Laden ,mwana wa Osama Bin Laden.
Ujumbe huo unaaminika kuwa wa kwanza wa propaganda za Al Qaeda kumshirikisha Hamza Bin Laden kama mwanachama wa kundi hilo.Katika ujumbe huo uliosambazwa na Al Qaeda katika mtandao wa twitter,Hamza Bin Laden anaagiza mashambulizi dhidi ya Marekani na washirika wake.
Osama bin Laden aliuawa na vikosi maalum vya Marekani mnamo mwaka 2011 katika uvamizi nyumbani kwake huko Abbotabad,Pakistan.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjma7dIUUeylqS0kEtXPmdeGoqSRKxFlYB3UI_YlVR_srvOgO1F59sRpfM6QbWzz64jsQbrD-LooSxIZR8gz5lkvdSNBTxRsAKih1uo8e2pkFkmcNdO5K_KA-wzmJ3_928Vl64H9wpjI3hf/s640/130130152046_zero_dark_thirty_624x351_ap_nocredit.jpg)
Wakati wa uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan mwaka 2001,shirika la habari la Al-Jazeera lilionyesha picha yake miongoni mwa wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan.
Ujumbe wake wa sauti uliotolewa na Al Qaeda unawataka wafuasi wake mjini Kabul,Baghdad na Gaza kuanzisha jihad ama vita vitakatifu mjini Washington,London,Paris na Tel Aviv
0 MAONI :
Post a Comment