
Jembe jipya la City Alvaro Negredo.
Dili la usajili wa mchezaji huyu lingeweza kukamilika mapema zaidi
lakini Sevilla na City zilishindwa kufikia makubaliano ya bei halishi ya
mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 27 .Usajili wa Negredo utakapokamilika utafanya idadi ya wachezaji walioko kwenye kikosi cha kwanza cha City ambao ni raia wa Hispania kufikia wachezaji watatu baada ya David Silva ambaye atakuwa anaichezea City kwenye msimu wake wa tatu na Jesus Navas ambaye alisajiliwa mapema majira haya ya joto akitokea huko huko anakotoka Negredo Sevilla .
Ujio wa Negredo ambaye alifunga mabao 31 kwenye michuano yote akiwa na Sevilla msimu uliopita huenda ukamfanya mshambuliaji Edin Dzeko kuangalia uwezekano wa kuondoka kwani utafanya nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha City kuwa finyu zaidi.
0 MAONI :
Post a Comment