Mkorea PSY ambaye wiki iliyopita video ya wimbo wake wa
Gangnam Style ilivunja rekodi YouTube baada ya kutazamwa zaidi ya mara
bilioni mbili, ameachia video ya wimbo wake mpya aliomshirikisha Snoop
Dogg unaitwa Hang Over.
Katika video hiyo, PSY na Snoop Dogg wanajaribu kuonesha madhara ya
kuamka na hang over ya pombe ambapo yanaonekana magari yakigongana
asubuhi kwa kuwa madereva wana hang over. Video imekaa kiucheshi kama
kawaida ya video za PSY.
Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
0 MAONI :
Post a Comment