Tangaza na Abd Da Hustler

Hizi ndio rekodi 5 za soka ambazo hazijawahi kuvunjwa katika historia ya soka …



Tukiwa tunaelekea kuuaga mwaka 2015 kuna mengi yametokea katika maisha ya soka, moja kati ya vitu vilivyotokea katika soka mwaka 2015 tumeshuhudia Jamie Vardy wa klabu ya Leicester City  akivunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Man United Ruud van Nistelrooy ya kufunga magoli 10 mfululizo.
Rekodi ambayo ilidumu kwa miaka 12 toka Van Nistelrooy aiweke. December 5 naomba nikusogezee rekodi za soka ambazo hazijawahi kuvunjwa toka zimewekwa, Stori kutoka sportskeeda.com hadi kufikia November 16 2014 ndio zilikuwa rekodi ambazo hazijawahi kuvunjwa katika soka.
1- Idadi ya mashabiki wengi wa soka kuingia uwanjani: Hii ni rekodi iliwekwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1950 katika mchezo kati ya Brazil dhidi ya Uruguay katika dimba la Maracanazo, mchezo ambao unatajwa kuingiza idadi rasmi ya watu 173,850 ila inatajwa kuwa idadi ilifikia hadi watu 210000 pamoja na wasio kuwa na tiketi.
World Cup Finals, 1950, Brazil, Rio De Janeiro, Aerial view of the gigantic Maracana Stadium still under construction for the 1950 World Cup finals  (Photo by Popperfoto/Getty Images)
2- Mechi iliyowahi kufungwa magoli mengi zaidi: Rekodi hii iliwekwa mwaka October 31 2002 katika mchezo ngazi ya vilabu kati ya AS Adema dhidi ya SO l’Emyrne uliyochezwa Madagascar. Mchezo ulimalizika kwa AS Adema kuibuka na ushindi wa goli 149 – 0 magoli ambay0 SO l’Emyrne walijifunga kwa makusudi baada ya mchezo uliyopita kutoridhishwa na maamuzi ya refa na kuwafanya wakose matumaini ya kutwaa Ubingwa. Baada ya mechi kocha wa SO l’Emyrne alifungiwa miaka mitatu na wachezaji wanne walifungiwa hadi mwisho wa msimu.
149-0-1416147447
3- Ali Daei kutokea Iran amewahi kucheza katika vilabu vya Bayern na Hertha BSC na timu ya taifa ya Iran, anashika rekodi ya kufunga idadi kubwa ya magoli katika mechi za kimataifa, amecheza jumla ya mechi 149 akiwa na Iran na kufunga magoli 109 katika miaka 13 yake ya kucheza soka.
4-1416145061
4- Licha ya kuwa Pele ndio anatajwa kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi 1375 kwa kila mechi, ila idadi ya mechi zake rasmi za mashindano zinatajwa kuwa 1115, golikipa Rogerio Ceni ndio mchezaji ambaye anatajwa kuwa amecheza mechi nyingi zaidi rasmi kuliko mchezaji yoyote, amecheza jumla ya mechi 1141. Ceni alikuwa akiichezea Sao Polo ya Brazil toka mwaka 1992. Rekodi ambayo inatajwa kaiweka akiwa na klabu moja na jumla ya mechi zake chache alizocheza timu ya taifa.
8-1416145035 (1)
5- Klabu ya Real Madrid ya Hispania ndio inatajwa kuwa na rekodi ya kuchukua Kombe la klabu Bingwa Ulaya mara tano mfululizo, imewahi kufanya hivyo mwaka 1955 na 1960. Licha ya kuwa Barcelona ya Guardiola na FC Bayern Munich ya Heynckes kutajwa kuwa bora haijawahi kutwaa taji hilo hata mara mbili mfululizo.
6-1416144968

Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment