Tangaza na Abd Da Hustler

HABARI NZURI TZ: Mchezaji wa Tanzania mwenye dili jipya la kuvalishwa viatu na kampuni ya PUMA

Soka la Tanzania linazidi kusogea na kuzipiga hatua za kimaendeleo na mastaa wake nao wanagonga vichwa vya habari kila kukicha, sasa hivi kiungo Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anakaribia kuingia mkataba na kampuni ya vifaa vya michezo ya Ujerumani utakaomuwezesha kupata vifaa vya michezo bure kutoka kampuni hiyo.

“Puma walikuwa wananifuatilia wanataka kunidhamini baada ya kuongea na wakala wangu, tutaingia mkataba wa kunidhamini kwa vifaa vya michezo hususani viatu, nilivyokuwa timu ya taifa Samatta alinishauri nikubali kudhaminiwa na PUMA na ni baada ya mimi kumuuliza” >>> Farid Musa.
Farid Musa mwenye mpira kulia

“Lakini kuna vitu pia Samatta kanishauri niwaambie viwemo kwenye mkataba, niliongea na bosi Yusuph kuhusu mpango huo akaunga mkono, kwa sasa bado nachipukia kuhusu kufaidika bado sijajua sana ila mimi malipo yangu itakuwa nikupewa vifaa na mimi kuvivaa nikiwatangaza, nikienda Ulaya ndio nitaanza kulipwa” >>> Farid

Farid tayari ameridhishwa na viatu vya Puma na kuvisifia viatu kama SL Boot na Evo Speed Faster kuwa ni vyepesi, kama huwa upo karibu na stori za sports, Puma wamekua wakifanya kazi na mastaa wa soka duniani na waliwahi kuingia mkataba wa pound milioni 5 wa kumdhamini mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya Manchester City Sergio Aguero.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment