Tangaza na Abd Da Hustler

Kenya na Tanzania zashuka orodha ya Fifa


Wachezaji wa Taifa Stars ya Tanzania

Kenya imeshuka hatua 12 nayo Tanzania ikashuka hatua 5 kwenye orodha ya viwango vya ubora wa soka ya Fifa iliyotolewa leo.

Kenya kwa sasa wamo nambari 115 nao Tanzania nambari 130.

Harambee Stars wameshuka baada ya kushindwa mechi mbili za kufuzu kwa Kombe la Mataifa Bingwa Afrika na Guinea Bissau.

Taifa hilo la Afrika Magharibi limepanda hatua 45 hadi nambari 102.

Guinea Bissau waliichapa Kenya 1-0 mechi ya kwanza tarehe 23 Machi na kwenye mechi ya marudiano wakashinda tena 1-0 jijini Nairobi.


Mchezaji wa Harambee Stars kwenye mechi ya awali

Tanzania hawajahesabiwa mechi yoyote ya karibuni. Walishinda 1-0 dhidi ya Chad mechi ya kwanza ugenini lakini Chad wakajiondoa na hawakushiriki mechi ya marudiano jijini Dar es Salaam. CAF ilifuta matokeo hayo dhidi ya Chad katika kundi G.

CAF: Chad yajiondoa, Tanzania mashakani

Miongoni mwa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uganda inaongoza ikiwa nambari 72, Rwanda inafuata nambari 87, Kenya nambari 115, Burundi nambari 122, Tanzania nambari 130 na Sudan Kusini nambari 155.

Orodha ya mataifa kumi bora Afrika ni kama ifuatavyo:

1. Algeria

2. Ivory Coast

3. Ghana

4. Senegal

5. Misri

6. Cape Verde

7. Tunisia

8. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

9. Guinea

10. Congo


Duniani, orodha ya kumi bora ni kama ifuatavyo:

1. Argentina
2. Ubelgiji
3. Chile
4. Colombia
5. Ujerumani
6. Uhispania
7. Brazil
8. Ureno
9. Uruguay
10. England
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment