Tangaza na Abd Da Hustler

Kwa wanaosubiri mchezo wa Yanga Vs Al Ahly ya Misri, kuna taarifa mpya hapa

Uongozi wa klabu ya Dar Es Salaam Young Africans leo April 6 kupitia kwa afisa habari wake Jerry Muro ameongea na vyombo vya habari na kuelezea taarifa za mchezo wao wa klabu Bingwa barani Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaochezwa April 9 2016 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

Jerry amethibitisha Al Ahly kuwasili Dar Es Salaam alfajiri ya leo, pamoja na CAF kutoa majina ya waamuzi wa mchezo huo ambao wanatoka Ivory Coast Denis Dembele, Mauris Donatien, Moussa Bayere, Tangba Kambou lakini kamisaa wa mchezo Celestine Ntangungira anatokea Rwanda.

Jerry Muro

Hadi sasa Yanga mechi zao zilizopita za klabu Bingwa Afrika waligoma zisioneshwe kwenye TV ” Kwa sasa viongozi wanafanya utaratibu wa kuangalia namna ambavyo tunaweza kuruhusu TV kuonesha mchezo huo, lakini watu wajue tutaruhusu matangazo ya TV yarushwe mikoani kasoro Dar na Pwania ndio maana tumeweka kiingilio cha chini elfu tano” >>> Jerry Muro

KAMA ULIKOSA KUTAZAMA VIDEO YA MAGOLI YA YANGA VS KAGERA SUGAR APRIL 3 2016
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment