Televisheni ya taifa ya Iran imesema kwamba vituo
vya kupigia kura vitakuwa wazi kwa saa mbili zaidi
kutokana na kujitokeza kwa idadi kubwa ya watu
wanaotaka kupiga kura.
Imesema kwamba kutokana na watu kujitokeza kwa
wingi maafisa wa uchaguzi wameomba kuongezwa
muda kwa saa mbili hadi hapo saa kumi na moja na
nusu jioni na kwamba waziri wa mambo ya ndani
Mostafa Mohammad Najjar amelikubali ombi hilo.
Baraza la Walezi linaloangalia uchaguzi huo
limesema hakukuwa na matatizo yoyote . Wizara ya
mambo ya ndani haikutowa takwimu zozote zile juu
ya idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura lakini kwa
mujibu wa waandishi wa habari wa AFP baadhi ya
vituo vya kupigia kura katika mji mkuu wa nchi hiyo
vilikuwa vimefurika wapiga kura.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 MAONI :
Post a Comment