Rais Barack Obama wa Marekani pia atakutana na
mpinzani mkuu wa Kansela Angela Merkel katika
uchaguzi mkuu ujao mbali na Kansela mwenyewe na
rais wa Ujerumani Joachim Gauck wakati wa ziara
yake nchini Ujerumani wiki ijayo.
Kwa mujibu wa taarifa ya serikali Obama ambaye
anatarajiwa kuwasili katika mji mkuu wa Ujerumani
Jumanne usiku akiandamana na mke wake Michelle
baada ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Kundi la
Mataifa Manane Tajiri duniani huko Ireland ya
Kaskazini atakutana na Peer Steinbruck mgombea wa
ukansela wa chama cha upinzani cha siasa za wastani
za mrengo wa shoto Social Demokratik SPD
Ikiwa ni miezi mitatu kabla ya uchaguzi mkuu hapa
nchini .
Merkel atampokea Obamba Jumatano asubuhi katika
ofisi ya kansela na baadae watakuwa na mkutano wa
pamoja na waandishi wa habari.
Syria,Afghanistan na Mashariki ya kati,mpango wa
nuklea wa Iran na mpango wa upelelezi wa mtandao
wa Marekani uliofichuliwa hivi karibuni yatakuwa ni
miongoni mwa agenda ya mkutano wao.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 MAONI :
Post a Comment