Tangaza na Abd Da Hustler

Jeshi la Mali ladhibiti mji wa Kidal

Msemaji wa jeshi la Mali Luteni Kanali Souleymane Maiga, amesema kwa mara ya kwanza wanajeshi wameingia mji wa Kidal ulioko kaskazini mwa nchi hiyo tangu walipoondolewa miezi 16 iliopita na waasi wa Tuareg na baadaye na jeshi lililokuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la Al Qaida.
Mji wa Kidal kama maeneo mengine kaskazini mwa Mali uliingia katika mikono mbali mbali ya waasi tangu mwezi Machi mwaka jana. Msemaji huyo wa jeshi amesema jeshi liliingia Kidal saa kumi na moja jioni hapo jana na kuelekea hadi katika kambi ya kwanza ya kijeshi mjini humo.
Wanajeshi hao waliandamana na wanajeshi wa Ufaransa kama walivyofanya walipoikomboa miji ya Gao na Timbuktu mwezi wa Januari mwaka huu.
Mji wa Kidal hapo awali ulikuwa unatawaliwa na waasi wa Kituareg ambao sasa wametia saini  makubaliano na serikali ya Mali, kuliwezesha jeshi hilo kurudi tena mjini humo.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment