Ghasia zaidi mjini Cairo
Umoja wa Africa umelaani hatua ya jeshi la Misri kumpindua Rais Mohammed Mursi. Sasa Umoja huo umeusimamisha uanachama wa nchi hiyo, huku ikitaka hali ya kikatiba irudishwe nchini humo na kuikumbusha Misri juu ya msimamo wake thabiti dhidi ya mabadiliko yanayoenda kinyume na katibaKatika mkutano wa Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika hapo jana kwenye makao yake makuu mjini Adis Ababa, Ethiopia, Umoja huo pia umesema kuondolewa madarakani kwa Mohammed Mursi maana yake ni kuchukuliwa kwa mamlaka na jeshi kinyume na sheria.
0 MAONI :
Post a Comment