Tangaza na Abd Da Hustler

Shambulizi la sumu laua watu 355 Syria

Shambulio la siku ya Jumatano linalodaiwa kuwa ni gesi ya sumu lililosababisha mamia ya watu kufariki wakiwemo watoto  liliongeza wasiwasi kwa jumuiya  ya Kimataifa na kuanza mazungumzo ya hatua ya haraka itakayochukuliwa dhidi ya  nchi hiyo.  Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa Angela Kane yuko mjini Damascus kuishinikiza serikali ya Syria kuwaruhusu wachunguzi wa Umoja huo kufanya uchunguzi katika maeneo yanayodaiwa kutumika kemikali za sumu.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel pia ametaka wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kuruhusiwa kuingia katika maeneo hayo mara moja.Rais wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa kukutana na washauri wake wakuu juu ya swala hilo huku Jordan ikipanga kufanya mkutano juu ya Syria wiki hii mjini Amman.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment