Rais wa Syria, Bashar al-Assad amesema hana wasiwasi na rasimu ya
azimio lililowasilishwa na Marekani, Ufaransa na Uingereza, kwenye Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa. Kituo cha televisheni cha China CCTV,
kimeripoti leo kuwa Assad amesema tangu Syria ipate uhuru wake, nchi hiyo
imekuwa ikizingatia mikataba yote iliyosaini. Amesema kuwa wataheshimu
kila kitu walichokubaliana, akitolea mfano jinsi serikali yake ilivyokubali
kusalimisha silaha zake za sumu chini ya udhibiti wa kimataifa. Amesema
hatua ya kupelekwa kwa rasimu ya azimio hilo, au kuzitaka Marekani na Urusi
kukubaliana kuhusu mpango wao, Marekani, Ufaransa na Uingereza zinajaribu
kujionyesha kwamba zimeshinda vita dhidi ya Syria, nchi ambayo ni adui yao.
Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
0 MAONI :
Post a Comment