Tangaza na Abd Da Hustler

Watu 81 wauawa Pakistan

Idadi ya watu waliouawa katika shambulio la kujitoa muhanga katika Kanisa nchini Pakistan, imefikia 81, huku Wakristu wakiandamana nchi nzima wakidai ulinzi zaidi. Shambulio hilo la mabomu lililotokea kwenye Kanisa la Watakatifu Wote, kaskazini-magharibi mwa mji wa Peshawar baada ya ibada ya Misa jana Jumapili, linaaminika kuwa baya kabisa dhidi ya jamii ya Wakristu walio wachache. Dokta Arshad Javed, amesema watu wengine 131 wamejeruhiwa katika shambulio hilo. Paul Bhatti, rais wa muungano wa jamii za watu wachache nchini Pakistan, amesema wanaamini kuwa shambulio hilo ni kitendo cha kigaidi. Bhatti ambaye aliwahi kuwa waziri wa maelewano ya kitaifa katika serikali iliyopita, amesema Wakristu sio walengwa pekee wa ugaidi, bali nchi nzima inaathirika na ugaidi.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment