Mshambuliaji Luis Suarez
amefunga bao katika mechi yake ya kwanza kwenye uwanja wa Anfield tangu
mwezi April kwa ushirikiano na mshambuliaji mwenzake Daniel Sturridge
kuiwezesha Liverpool kuibwaga Crystal Palace
Raia huyo wa Uruguayan, aliyetumikia kifungo cha
mechi 10 kwa kumngata beki wa Chelsea alifunga bao safi katika kipindi
cha kwanza akiwa anagaragara chini.
Kisha Sturridge akaziona nyavu baada ya kuwatatiza mabeki wa Palaca na baadaye nahodha Steven Gerard akamilizia kwa mkwaju wa peneti.
Ushindi huo unaiweka Liverpool kileleni mwa Ligi kuu ya England kwa pointi 16, moja mbele ya Arsenal na City katika nafasi ya tatu.
Newcastle na Cardif
Mfaransa Loic Remy alifunga mara mbili kuiwezesha Newcastle kustahamili mikiki mikiki ya Cardif iliyobadilika katika kipindi cha pili ikitafuta ushindi dhidi ya wageni.
Fulham na Stoke
Mashabiki wa Fulham walimzomea kocha wao kwa matokeo ya awali na hali mbovu inayoonyeshwa na klabu yao.
Lakini kocha Martin Jol alimleta mshambuliaji Darren Bent kutoka meza ya wachezaji wa ziada kuipatia Fulham bao pekee la ushindi na kumpunguzia dhiki kocha wake.
Kwingine Hull City iliendelea kudhibiti rekodi yake ya kutopoteza kwenye uwanja wa nyumbani na kuikwamisha Aston Villa ikiridhika kwa matokeo ya 0 -0.

0 MAONI :
Post a Comment