Tangaza na Abd Da Hustler

Wataalamu wa silaha za sumu wawasili Syria

Ujumbe wa wataalamu wa kuziondoa silaha za  sumu umewasili nchini Syria kuanza jukumu la  kuziorodhesha silaha hizo ili kuziteketeza hapo baadae.
Wakaguzi hao kutoka shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za sumu lenye makao mjini The Hague, OPCW waliwasili Syria kwa magari kutokea Lebanon, siku moja baada ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa, waliokuwa wanafanya uchunguzi juu ya madai ya kutumika silaha za sumu, kuondoka nchini Syria.
Wakaguzi hao wa shirika la OPCW wapo Syria kulitekeleza azimio la Umoja wa Mataifa linaloitaka Syria iziteketeze silaha zake za sumu hadi ifikapo kati kati ya mwaka ujao.
Syria inasemekana kuwa na tani zaidi ya alfu moja ya gesi za sarin na mustard na silaha za sumu za  aina nyingine zilizopigwa marufuku. Silaha hizo zimewekwa katika sehemu 45 tofauti nchini Syria kote.  
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment