Tangaza na Abd Da Hustler

Berlusconi ageukwa na wabunge wa chama chake

Aliekuwa Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi amegeukwa na wabunge kadhaa wa chama chake kuhusu njama zake za kutaka kuiangusha serikali ya mseto nchini Italia wakati pana wasiwasi kwamba mgogoro wa kisiasa katika nchi hiyo inayoshika nafasi ya tatu kwa nguvu za kiuchumi katika ukanda  wa sarafu ya Euro unaweza kusababisha athari  duniani kote.
Waziri mkuu huyo wa zamani Berlusconi alijitenga  na serikali ya Waziri Mkuu wa sasa wa Italia Enrico  Letta, baada ya washirika wa serikali ya mseto kukataa kuzuia taratibu za kumfukuza Berlusconi bungeni kutokana na mahakama kumtia hatiani kwa  udanganyifu wa kodi.
Berlusconi amepania katika mipango yake ya kumwangusha Waziri Mkuu Enrico Letta lakini  anazidi kugeukwa na baadhi wabunge wa  chama  chake ambao wamesema wataiunga mkono serikali ya Waziri Mkuu Letta.
Mpambe mwandamizi wa Berlusconi,Angelino Alfano ambae ni waziri wa mambo ya ndani amewaambia wabunge wa chama cha Berlusconi-PDL, wamuunge mkono Waziri Mkuu Letta kwa kumpigia kura ya kuwa na imani nae leo bungeni.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment