Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
amezitahadharisha nchi za magharibi juu ya
Iran na katika hotuba yake amezitaka nchi
hizo zisimwamini rais mpya wa nchi hiyo.
Akihutubia kwenye Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa Waziri Mkuu Netanyahu,pia alisema
kwamba Israel ipo tayari kuchukua hatua
peke yake ili kuizuia Iran kuunda silaha za
nyuklia.
Netanyahu aliwaambia wajumbe kwenye
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba
yeye hamwamini Rais Hassan Rouhani wa
Iran na kwamba mtu mwengine yeyote
hapaswi kumwamini Rais huyo.
Amesema Rais Rouhani ni mbwa mwitu
alievaa manyoya ya kondoo. Waziri Mkuu wa
Israel aliitoa hotuba hiyo siku moja tu baada
ya kukutana na Rais Obama kwenye Ikulu
ya Marekani ambapo aliitaka Marekani
iendelee kuishinikiza Iran.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 MAONI :
Post a Comment