Majeshi ya Amisom yamefanikiwa kufurusha Al Shabaab kutoka katikja ngome zao za Mogadishu na Kismayo
Mashirika ya kutoa misaada,
yalitozwa pesa na wanamgambo wa Al Shabaab ili yaweze kuruhusiwa kuingia
katika maeneo waliyokuwa wameyadhibiti, wakati wa janga la njaa mwaka
2011.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa taasisi mbili za utafiti barani Afrika.Baadhi ya mashirika hayo yangali yanalipa Al Shabaab ili yaruhusiwe kuingi katika maeneo ambayo watu wanahitaji msaada nchini Somalia na hasa maeneo ambayo bado kundi hilo linadhibiti.
Zaidi ya watu 250,000 walifariki wakati wa janga hilo mwaka 2011.
Ripoti hiyo iliyotolewa na taasisi ya kimataifa ya maendeleo na ustawi pamoja na taasisi nyingine ya sera mjini Mogadishu, ilitaja pesa hizo kama malipo ya usajili na mashirika hutozwa hadi dola 10,000 za kimarekani.
Taasisi hizo zinasema kuwa wakati mwingine al-Shabab ilichukua chakula kilichonuiwa kupelekewa watu kama msaada katika mji wa Baidoa,.
0 MAONI :
Post a Comment