Tangaza na Abd Da Hustler

Azam,Mbeya City,Yanga kuachuana leo kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania


LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inaendelea leo ambapo Coastal Union wanaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000 na sh. 15,000. Nayo Ruvu Shooting na Mbeya City zitapambana kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani kwa viingilio vya sh. 10,000 na sh. 5,000.
Huku uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mtibwa Sugar.Viingilio ni sh. 5,000 na sh. 3,000.
Azam itaumana na Rhino Rangers katika Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Mbagala.Viingilio ni sh.10,000 na sh. 3,000.
Yanga SC ambao ndio mabingwa watetezi, wanaongoza Ligi Kuu kwa pointi zao,31 wakifuatiwa na Azam Mbeya City zenye 30 kila moja baada ya timu zote kucheza mechi 14.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment